Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba wakati ufungaji wa wiki ya akifunga wiki ya Habari ya Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma(SJMC) katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dares Salaam iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho.
Mlemavu wa miguu wa Kundra Mazingera aliyeketi katika akionyesha umahiri wa kupiga gitaa wakati ufungaji wa wiki ya akifunga wiki ya Habari ya Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma(SJMC) katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho. Kushoto ni mpiga ngoma wa kikundi hicho Ibrahim Haji na nyuma ni Muhaza Mwalimu wote wa kikundi cha cha Lumbumba Theater.
Na.Magreth Kinabo – Maelezo
Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi amewataka wanataalama walio kwenye taasisi za kiserikali kushiriki katika usimamizi wa vyombo vya habari ili visidondoke mikononi mwa wasioitakia mema tasnia ya habari, huku akitaka tatizo la makanjanja litafutiwe ufumbuzi..
Aidha alisema serikali inahitaji sekta ya habari iliyo imara na yenye kutumainiwa kwa ustaawi na usalama wa taifa .
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Nchimbi wakati akifunga wiki ya Habari ya Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma(SJMC) katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dares Salaam iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho.
“Sekta ya habari imepanuka kwa ukubwa na mawanda, huku ni kukaribisha maendeleo.Hata hivyo inahuzunisha kuona kwamba suala hili linafungua milango kwa makanjanja kuvamia tasnia hii. Kinachonitia moyo ni kuona kwamba wengi wa wataalamu wetu katika tasnia hii wamesimamia weledi na maadili.
“ Tunatarajia kuona SJMC ikibaini mianya hii na kuitafutia ufumbuzi na kuhakikisha kuwa wale wote wanaopita kwenye tanuri lake wanaokwa na kuiva kabisa tayari kwa kuchangia maendeleo ya taifa,” alisema Waziri Nchimbi.
Waziri Nchimbi alisema serikali itahakikisha rasilimali zote muhimu zinapatikana ili kuwezesha SJMC kuwa kituo bora kitalaama.
Alitoa changamoto kwa SJMC, kuwa isiishie kuwa kisima cha maarifa, bali inapaswa kanuni, tamaduni na maadili ya uandishi wa habari.
“Ongezeni kufundisha misingi ya utamaduni katika kulitumikia taifa. Ni matarajio ya serikali kuona kwamba wahitimu wenu wanawajibika ipasavyo katika kulitumikia taifa huku wakiweka mbele maslahi ya taifa,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa wataalamu wa fani ya habari na wanafunzi wa chuo hicho kushughulikia matukio na shughuli mbalimbali zitakazoweza kubaini fursa na vipawa walivyonavyo watu hususan maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake Mkuu wa SJMC, Dk.Bernadetta Killian alipendeleza kuwa na mkutano wa pamoja wa wataalamu wa tasnia hiyo ili kuweza kuifanya taaluma kwa vitendo na kuongeza ujuzi. aliongeza kuwa ili kulitekeleza suala hilo mchango wa hali na mali unahitajika.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Raphael Hokororo aliwataka waandishi wa habari kuheshimu taaluma yao na kukubali kujifunza , ikiwemo kuandika habari za kweli.
Habari kwa hisani ya Mo Blog
No comments:
Post a Comment