Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, June 26, 2011

WALANGUZI UFUTA KILWA KUKIONA:NAPE…!!!

- Amtaka mbunge CUF arudi bungeni,aache ulanguzi.

-Madiwani wa CCM wakithibitika kuhusika kutimuliwa.



Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa (MNEC) Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa hadhara mkoani Lindi.

NA.BASHIR NKOROMO, LINDI
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, ametangaza kiama cha walanguzi wa ufuta kwa kuitaka serikali ya wilaya ya kilwa na mkoa wa Lindi kuhakikisha inakomesha ulanguzi huo mara moja.

Nape alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika mji mdogo wa Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko katika ziara ya siku mbili ya baadhi ya wajumbe wa Sekretariti ya CCM mkoani Lindi katika kufikisha ujumbe wa maamuzi ya NEC yaliyofanyika mjini Dodoma Aprili mwaka huu.

Nape alisema kinachoendelea kwa walanguzi wanaokwepa mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye ununuzi wa ufuta ni hujuma kwa wakulima na serikali ya CCM kama mtetezi wa wanyonyonge hasa wakulima haiwezi kukaa kimya na kuangalia wakulima wakidhulumiwa haki zao.

Kwa mujibu wa Nape wapo viongozi wa kisiasa wanaongoza dhuluma hiyo kwa kisingizio cha kuwasaidia wakulima wakati ukweli wanawadhulumu na kumshushia tuhuma hizo mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungala ‘Bwege’ kuwa ndio kinara dhuluma hiyo. “naambiwa mbunge wenu bwana ‘Bwege’ kaacha bunge la bajeti na kuja kusimamia dhuluma yake dhidi ya wakulima masikini wa ufuta. Bwege rudi bungeni kama hujui kazi yako ni kuwatetea wananchi basi bora ujiuzulu wananchi wapate mwakilishi na si mlanguzi” alisema Nape.

Alisema wakati bei ya dira mwaka huu ni sh. 1000 ambayo serikali iliagiza mkulima alipwe yote ndio asubiri malipo ya pili ambayo nayo yatakuwa mazuri kwani bei ya ufuta safari hii ni nzuri, walanguzi wananunua ufuta kwa kati ya sh. 1,150 na sh. 1,200 ambayo ni wizi kwa wakulima.

Akifafanua wizi huo Nape alisema, ushahidi wa wazi uliopo walanguzi wamechezea mizani yao na kwa kila kilo moja wanaiba kati ya robo na nusu kilo na hivyo bei ya sh. 1200 wanayonunua walanguzi ni danganya toto kwani tayari wameshafidia kwenye mizani za wizi. “mizani za vyama vyetu vya ushirika imepimwa na wakala wa vipimo hivyo ni sahihi na tayari serikali yenu imesha simamia upatikanaji wa bilioni kumi na moja kutoka benki za NMB na CRDB kwa ya ununuzi wa ufuta msimu huu, hivyo hakuna sababu ya wakulima wa ufuta kuendelea kudhulumiwa na hawa matapeli” Alisisitiza Nape.

Alisema kuendelea kukwepa mfumo wa stakabadhi ghalani ni kwenda kinyume na maamuzi ya RCC, ambacho ni kikao halali na hata baraza la madiwani ambao ni wawakilishi halali wa wananchi.

“Naambiwa wako na baadhi ya madawani wa CCM wanaojihusisha na dhuluma hii, naagiza ushahidi ukipatikana vikao vya chama mchukue hatua kali dhidi yao, tuko tayari kufanya uchaguzi mdogo kuliko kuvumilia dhuluma hii, alisema Nape.


Mapema, Nape na Asaha walizungumza na viongozi mbalimbali wa chama wakiwemo wajumbe wa nyumba kumi.

Akizungumza na viongozi hao Nape alieleza kwa kina lengo la hatma ya CCM kufanya mabadiliko ‘kujivua gamba’ mjini Dodoma na kwamba moja ya malengo ni kukirejesha chama kwenye misingi yake ili kiweze kikidhi kwa dhati matarajio ya wananchi hasa wanyonge.

Nape alisema katika hatua hiyo, Chama sasa kimeongeza nguvu zaidi ya kuisimamia serikali iwaheshimu na kuwatumikia wananchi na kuwa kukifanya Chama kuwa cha wanyonge.

Kwa upande wake, Katibu wa NEC, Oganazesheni, Asha Abdallah Juma ambaye amefuatana na Nape katika ziara hiyo, aliwataka viongozi wa CCM hadi ngazi za wajumbe wa nyumba kumi kurejesha heshima ya Chama.

Aliwataka viongozi na wanachama wa CCM kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa uanachama ikiwemo kutoa ada za uanachama kama inavyotakiwa.

Pamoja na Asha, katika ziara hiyo pia Nape ameambatana na Katibu Msaidizi Mkuu Itikadi na Uenezi Sixtus Mapunda.

No comments: