Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, June 27, 2011

shaggy atinga kijiji cha makumbusho ya wasukuma Bujora,asimikwa ubalozi wa kabila hilo.


Haaa haaaa ka Mfalme Mswati vile..! Shaggy akiondoka viwanjani hapo huku akinesa nesa kiaina,wakati huo huo akisindikizwa na vimwana mara baada ya hafla hiyo fupi ya kusimikwa kufikia kileleni.
Mwanamuziki Shaggy akionekana mwenye furaha,huku akishangilia mara baada ya kusimikwa ubalozi wa kabila la Kisukuma,na baadhi ya wazee wa kabila hilo,ambapo leo walikuwa wakisherehekea siku yao ya mavuno (Bulabo) ambayo imeanza leo tarehe 26 juni na itakoma julai 3,katika viwanja hivyo vilivyo maeneo ya Kisesa jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Bodi ya SBL,Mzee Jaji Mark Boman akizungumza machache mara baada ya mwanamuziki Shaggy kusimikwa ubalozi wa Kabila la Kisukuma na Wazee maarufu wa kabila hilo.
Chifu Charles Kaphipa akizungumza katika tamasha hilo la Bulabo kabla ya kumtawaza mwanamuziki Shaggy kuwa balozi wa kabila hilo, wanaosikiliza kutoka kulia ni Chifu Makwaiya, Meneja wa Serengeti Allan Chonjo, Mkurugenzi wa Masoko (SBL) Caroline Ndungu,Mwanamuziki Shaggy pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya SBL,Jaji Mark Bomani.

Mwenyekiti wa Bodi ya SBL,Mzee jaji Mark Bomani akiteta jambo na Mwanamuziki Shaggy.

Mwanamuziki Shaggy akiwaimbia moja ya wimbo wake mbele ya baadhi ya watu waliofika kwenye hafla hiyo fupi ya kushuhudia kusimikwa Ubalozi kwa mwanamuziki huyo.
wacha wee palinoga ile mbaya .! Wageni wakiwasili huku wakipokelewa kwa heshima na adabu.

Shaggy akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mzee Pius Ng'wangu wakati alipofika hapo katika makumbusho ya Bujora.

Pichani kushoto ni Padre Fabian Mhoja akimkaribisha Mwanamuziki Shaggy ndani ya kijiji cha makumbusho ya Wasukuma,alipokwenda kutembelea na kujionea mambo mbalimbali ya tamaduni ya kabila la Kisukuma,Wa pili kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Serengeti Allan Chonjo,Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya SBL,Jaji Mark Bomani,Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Caroline Ndugu pamoja na Meneja Matukio wa SBL Bahati Singh.

Mwanamuziki Shaggy akisindikizwa na vimwana mara alipowasili kwenye uwanja ambao sherehe za Kisukuma 'Bulabo'zilipokuwa zikifanyika.
Shaggy akifanunua jambo mbele ya waandishi wa habari,kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Serengeti Breweries Ltd Caroline Ndugu,na kushoto ni Meneja mawasiliano ya ndani ya SBL,Iman Lwinga pamoja na Meneja wa kinywaji cha Primeum Serengeti Lager Allan Chonjo.
Mwanamuziki Nguli kutoka nchini Marekani,Shaggya akiwa na wenyeji wake (Wadhamini) kutoka kamouni ya Bia ya Serengeti (SBL), alipokuwa akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari mbalimbali,kwenye mkutano uliofanyika mchana katika hoteli ya Malaika iliopo nje kidogo ya jiji la Mwanza

Habari kwa hisani ya Jiachie Blog

No comments: