Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, June 24, 2011

RC MBEYA AWATOLEA UVIVU WANASIASA WANAOCHOCHEA WANANCHI KUIPUUZA SERIKALI


Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mbeya Bw.Joachim Nyambo anaripoti kuwa serikali mkoani Mbeya imewatolea uvuvi wanasiasa wanaowapotosha wananchi kukaidi agizo la serikali la kukubali kuhama
katika vijiji vinavyopaswa kupisha hifadhi ya taifa ya Ruaha katika
eneo la Ihefi wilayani Mbarali.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya John Mwakipesile amewasihi wananchi kutowasikia
wanasiasa uchwara hao akisema lengo lao si kutetea maslahi ya taifa
badala yake maslahi binafsi wakidhani kufanya hivyo ndiyo njia ya
kuziteka kura za wananchi.

Mwakipesile alisema utekelezaji wa agizo hilo utakapoanza, ni lazima
zitakuwepo siasa kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, kuwataka wananchi hao
wasiondoke katika vijiji hivyo kwa madai kuwa ni kulinda haki za
binadamu.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa changamoto hiyo katika mkutano wa Machifu,
wazee maarufu, wenyeviti na watendaji wa vijiji vinavyotarajiwa
kuhamishwa jifadhi ya Ruaha, eneo la bonde oevu la Ihefu uliofanyika
wilayani hapa.

“Nina uhakika mara baada ya zoezi hilo la upanuzi wa hifadhi kuanza
kwa kuhamisha wananchi katika baadhi ya vijiji vilivyopo jirani
watajitokeza baadhi ya wanasiasa.Wananchi hawapaswi
kuwasikiliza.Watawarubuni kuwataka wasikubali kuondoka kwa madai kuwa
haki za binadamu, mna haki ya kisheria kuishi, lakini mwisho wa siku
ni vyema mtambue umuhimu wa eneo hili la bonde oevu la Ihefu kwa
vizazi vijavyo” alisema

Aliitaka pia kamati ya kusimamia zoezi hilo la uhamishwaji wa wananchi
katika vijiji hivyo vinavyotarajiwa kuhamishwa, kutumia hekima zaidi
kuliko nguvu, na kufafanua kuwa hilo litafanikiwa iwapo wananchi
watapewa elimu sahihi juu ya uamuzi huo wa serikali.


Aliongeza bonde la Usangu lina mchanganyiko wa watu kutoka mikoa
tofauti nchini, hivyo serikali imeona walizungumze suala hili kwa
kutumia busara, na kuwa ni lazima zitakuwepo siasa kwa baadhi ya
wanasiasa kutaka kuwadanganya, hivyo wawe nao makini.

Akifafanua zaidi juu ya mipaka mipya ya hifadhi hiyo Mwakipesile
alisema katika vijiji vilivyopo jirani na hifadhi,vijiji vya Luhanga,
Namagigiwe, vitongoji vya Ifushiro, Image na hekta 3,600 zilizopo kata
ya Madibira zilizoamriwa na rais
Jakaya Kikwete ziachwe kwaajili ya
matumizi ya wananchi ,ndivyo vitaondolewa katika hifadhi ya Ruaha na
kuachwa kwa wananchi lakini kutakuwa na uangalizi maalum ili
kuhakikisha mazingira yake hayaharibiwi.

Mmmoja wa waliohudhuria mkutano huo,Chifu wa kabila la Wasangu, Salehe
Merere, alisema umoja, mshikamano na kusimamia yale yaliyoafikiwa
ndani ya vikao, ndio njia pekee ya kufanikisha kulinusuru eneo hilo
oevu dhidi ya uharibifu wa mazingira.

Chifu Merere aliwataka wajumbe wa kikao hicho, kuacha tabia ya kugeuza
maadhimio yanayofikiwa kutofanya na wengi na kwenda kueleza tofauti
kwa wananchi kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha maafa na
malumbano yasiyo na msingi na kukwamisha malengo ya serikali.

HABARI KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN


No comments: