Meneja wa KCB Tawi la Mwanza, Walter Lema akipanda mti aina ya mparachichi katika Shule ya Msingi Tumaini iliyoko eneo la Kigoto wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza, huku walimu, wafanyakazi na wanafunzi wakishuhudia tukio hilo ambapo jumla ya miche ya miti 750 ilipandwa katika eneo la shule hiyo.
Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Misingi Tumaini, Wilhard Kamanzi akimwonyesha maeneo ya shule hiyo Meneja wa KCB Bw. Walter Lema (kushoto).
Mgeni rasmi katika tukio la Wiki ya Upandaji Miti kwa Benki ya KCB, Bw. Francis Mkabenga ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza akipanda mti katika Shule ya Sekondari Luchelele akishuhudiwa na wanafunzi wa shule hiyo. Jumla ya miche ya miti 750 ilipandwa katika eneo la shule hiyo.
No comments:
Post a Comment