Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, June 24, 2011

fly 540 kwa raha mustarehe. Big up wadau

Tayari tuko ndani ya jiji la Mwanza mapema asubuhi ya leo tukitokea jijini Dar, tumetumia takribani dakika 75 tu kwa kazi nzuri ya Rubani a.k.a Kapten Waweru wa ( pichani kushoto) FLY540 akiwa sambamba na mwenzake, kama wanavyoonekana na nyuso zao za tabasamu kwa kazi yao nzuri ya kuwasafirisha abiria wanaotumia usafiri wa kampuni hiyo katika maeneo mbalimbali Tanzania na Afrika Mashariki kwa raha mustarehe kabisa.

Kuwahi kwetu jijini Mwanza ni kwa madhumuni makubwa ya kuwaletea matukio mbalimbali yatakayokuwa yakihusiana na tamasha kubwa la burudani hapa nchini ambalo kwa sasa linatimiza mika kumi,tangu kuanzishwa kwake,si lingine ni Serengeti Fiesta 2011,ambapo katika uzinduzi wa kilele cha tamasha hilo mwanamuziki nyota kutoka nchini Jamaica/Marekani atazikonga nyoyo za wakazi wa jiji la Mwanza siku ya Jumapili ndani ya Uwanja wa CCM-Kirumba,ambapo pia wakazi wa jiji hilo watasherehekea Msimu wa Dhahabu unaoendelea wa miaka 10 ya Serengeti Fiesta 2011.


Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Fly 540 wakishoo love mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege,mapema leo asubuhi jijini Mwanza,Ndege za kampuni hiyo zinafanya safari za Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar, Mtwara na Mombasa, lakini pia kuwa upande wa Kenya inafanya safari katika miji ya Nairobi, Mombasa. Kisumu, Malindi, Lamu, Eldoret,Kitale, Mara, Diani, Kakamega, Meru, Nanyuki, Amboseli na Seronera.

Mie nikishuka asubuhi hii ndani ya Uwanja wa ndege wa jiji la Mwanza,yaah hali ya hewa sio mbaya sana ni ubaridi ubaridi hivi na manyunyu ya mvua ya hapa na pale,lakini kwa ujumla mambo yako safi kwa sababu kanaonekana kajua kanaanza kuchomoza chomoza hivi.

Mdau wa FullshangweBlog,Johnn Bukuku nae ametia timu na kitu cha Fly 540 mapema leo asubuhi kuliendeleza libeneke la kuwahabarisha wadau mbalimbali kuhusiana na matukio ya Msimu wa dhahabu unaoendelea na Serengeti Fiesta 2011.
Ndege ya Fly 540 ilipokuwa ikikata mawingu urefu wa futi elfu 30000 kutoka usawa wa bahari.
Habari kwa hisani ya Jiachie Blog

No comments: