Na Nova Kambota
Hakunaubishi kuwa jamii yetu ya kitanzania inazidi kuwa ya kipuuzi kadri sikuzinavyokwenda na kundi linaloonyesha kuzidiwa nguvu na ujinga ni kundila vijana huku ujinga wao wakiubatiza jina la “mambo ya kisasa” lakiniukitazama kiundani unabaini kuwa ni ulimbukeni wa kupenda tamaduni zakimagharibi na
pengine uzuzu wao na mdumao wa ubongo ikiwa ni matokeo ya kutopenda kufikiri.
Nimelazimikakutumia maneno makali sana leo kutokana na jambo ninalotakakulizungumzia hii leo kuwa ni zito sana na hili si lingine bali nikitendo cha mtanzania mwenzetu mwanadada Bhoke kufanya ngono namshiriki mwenzake Ernest huko nchini Afrika kusini katika jumba la BigBrother Africa, naam! ni kitendo kilichovuta hisia za watanzania wengiwalio ndani ya nchi na walio nje ya nchi, nataka kumshauri Bhoke kamakijana mwenzangu tena hadharani ukizingatia kitendo chake hikokimeonekana hadharani na zaidi ya yote nataka kumwambia ukweli pasipokupindisha neno kwa kiwango ambacho na uhakika marafiki zake hawawezikumwambia kwa kumwonea aibu, mimi nitamwambia leo pasipo kumung’unyamaneno.
Baadaya kurejea nyumbani Bhoke amenukuliwa akisema kuwa hakutumwa nawatanzania Afrika kusini bali alienda mwenyewe , ingawaje mara yakwanza nilivyosikia upuuzi huu nilidhani ni maswala ya kuuza gazeti tulakini kutokana na kusubiri kuona iwapo Bhoke mwenyewe atakanusha nahakufanya hivyo basi hakuna ubishi kuwa Bhoke amesema upuuzi huu ambaobilashaka badala ya kumjenga unazidi kumharibia yeye na mabinti wenginelakini mbaya zaidi unazidi kuwachafua vijana wa taifa hili, naam! Bhokeamefanya upuuzi na sasa ameongea ujinga.
Kwanzakabisa Bhoke hana sababu ya msingi ya kujitetea kutokana na kitendo chaaibu alichokifanya, ikumbukwe kuwa alipokuwa Afrika kusini Bhokealitambulika kuwa anatoka Tanzania na tangu akipanda ndege kuelekeahuko hakuna ubishi kuwa alikwenda kuwakilisha nchi yetu kwenye tasniaya burudani kama wafanyavyo wasanii na wanamichezo wengine hivyo kauliyake kuwa hakutumwa na watanzania haina mashiko na zaidi ni ya kitotokuliko uhalisia, labda nimwulize Bhoke swali moja tu rahisi, je kwaniniRichard aliposhinda alipokelewa kama shujaa? Au kwanini Mwisho nayealipongezwa na watanzania? Au basi iwapo yeye Bhoke angeshinda jeangekataa kupokelewa na kupongezwa na watanzania? Kwasababuhawakumtuma? Natoa changamoto kwa Bhoke ajifunze kuongea mambo yenyemantiki sio kutujia na vijisababu vya kitoto ambavyo havijai hatakwenye kiganja.
HiviBhoke anataka kutuambia kuwa yeye yuko sahihi? Na sisi tunaolaanikitendo chake ni washamba? Au tuna mambo ya kizamani? Au basi nanikamwambia Bhoke usasa ni kujidhalilisha na kutuvua nguo watanzania kamaalivyotufanya? Nani kamwambia Bhoke kuwa kufanya ngono hadharani nijambo linalokubalika kwa mila zetu? Mbona Bhoke anataka kutuchezeaakili kwa kutetea ujinga? Tena mchana kweupe! Bhoke anapaswa kutambuakuwa watanzania sio watumwa wa mila za kishenzi za kufanya ngonohadharani za watu wa magharibi?
Uzitowa jambo alilolifanya Bhoke hauwezi kuelezewa kwa misamiati walamethali , hata tujitahidi kuupaka mafuta kwa kiasi gani bado utabaki niutumbo wa aina yake kwa mwaka huu wa 2011 na pia itabaki katikakumbukumbu za watanzania kama aibu kubwa huu ndiyo ukweli ambao naonaBhoke anataka kuupindisha kwa hoja nyepesi mno tena zilizopwaya sana za“sikutumwa na watanzania”. Chukulia mfano video ya Bhoke ya huko Afrikakusini niliulizwa na rafiki yangu aishiye nchini Finland kuwanimeshaiona? Mimi kwa kuona aibu nikaficha na kusema hapana sijaiona,rafiki yangu hakuchukua muda akanitumia, hiki ndicho alichotufanyaBhoke duniani kote sasa wanamtambua kwa aibu yake hiyo!
Watanzaniani watu tuliokuzwa katika utu ikiwa ni pamoja na kuvumiliana nakusameheana ila ni kwa wale waliotayari kukiri makosa yao , kujutia nakuomba msamaha sasa tulitegemea Bhoke ajutie kosa lake na kuombamsamaha kwa watanzania lakini sasa yeye anataka kutupanda kichwani hukuakijua wazi kuwa ametuaibisha, hili halikubaliki hata kidogo ni lazimatumkemee vikali tena kwa maneno makali pasipo huruma, baada yakujidhalilisha yeye na kutuaibisha watanzania sasa Bhoke anatakakutudhihaki? Hili halikubaliki kabisa!
Ikumbukwekuwa Bhoke sio binti tu wa kitanzania bali ni msichana wa kitanzaniaaliyejijengea heshima kubwa kutokana na harakati zake kuhusu vijanakupitia kipindi cha 5 connect katika kituo cha EATV si hivyo tu kunabaadhi ya mabinti wadogo walikuwa wakimwona Bhoke akiendesha kipindihiko walijisemeza moyoni kuwa na wao siku moja wangetamani kuwa kamaBhoke naam! Bhoke alikuwa msichana wa kupigiwa mfano miongoni mwawasichana wenzake na vijana wa kitanzania kwa ujumla.
Bhokenayemjua mimi sio Bhoke huyu anayejibu upuuzi wa kitoto wa “sikutumwana watanzania” mimi namfahamu Bhoke jasiri ambaye ni aina ya mabintiambao hata ukienda naye hotelini hataki ofa za bure bali wewe utalipanusu nayeye atalipa nusu, huyu ndiye Bhoke nayemfahamu mimi ambaye kilajumatano nilikuwa naacha shughuli zangu kumwangalia naam! ni Bhokeniliyetamani siku moja nimhoji au nifanye naye kipindi. Lakini sasaBhoke anazidi kujibomoa kwenye mioyo ya watanzania, Bhoke anajaribukutikisa kiberiti afahamu hasira za watanzania, Bhoke anafanya mzaha namila zetu na hisia zetu.
NamtakaBhoke afikirie tena juu ya kosa lake na matamshi yake nayoyaita ni yakipuuzi kabisa“sikutumwa na watanzania” natoa changamoto kwa Bhokeajaribu kuomba ushauri kwa viongozi wake wa dini juu ya kitendo chakena kisha ajipange kwa hoja zenye mashiko na zitakazopooza hasira zawatanzania , aachane na porojo za kitoto kama ambazo ameanza kuziteteabadala yake namtaka Bhoke akumbuke yeye ni nani? thamani yake ni nini?na amefanya nini? naam! natoa wito kwa dada yangu Bhoke alitazame kosalake kwa jicho la tatu na akili ya kiutu uzima……….Tafakari! Allutacontinua!
Nova Kambota Mwanaharakati,
June 23, 2011,Tanzania East Africa
0717 709618 au +255717 709618
No comments:
Post a Comment