Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, May 7, 2011

Ujenzi wa uwanja mpya wa Ndege wa kimataifa Jijini Mbeya waendelea kwa kasi

  
Sehemu ya kusubiri kabla ya kusafiri ikiwa tayari imekamilika pamoja na eneo la mitambo ya kuongoza ndege ikiwa tayari.

Shehena la Mchanga na kokoto likiwa tayari kwa shughuli za ujenzi wa njia za kupitia ndege hizo

Mitambo Maalum kwa ajili ya ujenzi ikiwa imetua kutoka nje.
Lile swali ambao wadau wengi walikua wanalalamika kwamba uwanja wa ndege wa kimataifa ulioko Jijini Mbeya maeneo ya Songwe hauendi sasa majibu yake ndio kama yanavyo onekana hapo juu ambapo kazi ya ujenzi inaendelea kwa kasi ya ajabu,Kamera yetu ilijaribu kuonana na wakuu wahusika wa ujenzi wa uwanja huo lakini haukufanikiwa kutokana na kuwa na majukumu  mengi, hata hivyo tulifanikiwa kuwapata wafanyakazi wachache ambao walidai kuwa kasi ya uwanja si mbaya sana na wamepewa msisitizo ili  upate kukamilika kwa muda muafaka. Tutazidi kuwaletea maendeleo zaidi ya Ujenzi huu.

No comments: