Mnajimu na Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein amefariki dunia asubuhi hii jijini Dar es Salaam. Chanzo chetu cha habari ndani ya ofisi ya Sheikh Yahya kimesema mtabiri huyo amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitali ya Ukombozi iliyopo Morocco, jijini. Sheikh Yahya amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na aliwahi kwenda India kwa matibabu. |
1 comment:
kifo chake ni mwisho wa enzi za kuongoza nchi kichawi na vitisho vya kufa. ni mwisho wa nguvu za giza kuingia sehemu takatifu. ni pambazako na nuru ya taifa jipya la tanzania.
Post a Comment