Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, April 22, 2011

Wananchi wa Tanzania wachangiwa vifaa vya afya pamoja na madawa yenye thamani ya shilingi bil. 4.5

Na Anna Nkinda – Phoenix, Arizona
22/04/2011 Taasisi inayoshughulika na utoaji wa huduma za kibinadamu ya  Project C.U.R.E ambayo makao yake  makao makuu ni Colorado nchini Marekani imeichangia Tanzania kupitia Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete vifaa vya afya pamoja na madawa vyenye thamani ya dola za kimarekani milioni tatu sawa na shilingi bilioni 4.5 za kitanzania.
Taasisi hiyo ambayo iliamua kufanya harambee ya kuunga mkono jitihada za Mama Kikwete za kupambana na tatizo la vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga litatuma nchini  makontena matano yenye vifaa hivyo.
Kabla ya kutuma vifaa hivyo ambavyo vitasambazwa katika Hospitali na kliniki wataalamu kwa afya kutoka Project C.U.R.E watakuja nchini kufanya tathimini ya vifaa vinavyohitajika katika Hospitali na Kliniki ambazo zitakuwa zimependekezwa na wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.
Akiongea na wageni ambao walihudhuria katika hafla hiyo ya uchangishaji iliyofanyika jana mjini Phoenix,  Mama Kikwete alisema kuwa hivi sasa nchini Tanzania idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto vinavyotokana na tatizo la uzazi limepungua hii ni kutokana na jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na wadau mbalimbali wa afya katika kukabiliana na tatizo hilo.
Kuhusina na vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa WAMA alisema kuwa vifo hivyo vimepungua kutoka 147 kati ya vizazi hai 1000 kwa mwaka 1999 hadi kufikia 81 kati ya vizazi hai 1000 kwa mwaka 2009/10.
Mama Kikwete alisema, “Kwa upande wa vifo vya watoto wachanga navyo vimepungua kutoka  99 kwa kila vizazi hai 1000 kwa mwaka 1999 na kufikia 51 kwa kila vizazi hai 1000 kwa mwaka 2009/10 kama hali hii itaendelea tuna uhakika wa kufikia malengo namba nne na namba tano ya Milinia ifikapo mwaka 2015”.
Aliendelea kusema kuwa tatizo wanalokabiliana nalo katika kufanikisha uzazi salama ni ukosefu wa vitendea kazi, madawa na upungufu wa wafanyakazi katika sekta ya afya.
“Ninawaomba muweze kuisaidia Serikali ya Tanzania ili iweze kukabiliana na changamoto hizi kwani Serikali peke yake bila ya wafadhili haiwezi kumudu matatizo haya”, aliomba.
Baadhi ya wageni ambao walishiriki katika Harambee hiyo ilihudhuriwa na watu wapatao 1200 walisema kuwa baada ya kuisikia hotuba iliyotolewa na Mke wa Rais wameshawishika kuchangia katika kusaidia juhudi za serikali ya Tanzania za kutoa huduma bora ya afya kwa kila mwananchi na hasa wanawake na watoto ili kuweza kufikia malengo ya milinia namba nne na tano ifikapo mwaka 2015.
Kila mwaka Project C.U.R.E ambao wanafanya kazi zao katika  nchi 120 Duniani huwa wanamchagua mke wa rais mmoja kutoka katika nchi ambazo zinahitaji kusaidiwa na kumfanyia  harambee kwa ajili ya kumchangia vifaa vya afya na madawa. Tayari wameshafanya harambee kwa wake wa rais wa El Salvador, Belize, Mexico, Ghana na Panama.

No comments: