Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, April 23, 2011

Tafakuri yangu ya Leo:Taifa letu halilindi watu wake


  Jana usiku nilipata simu kutoka kwa mmoja wa wasomaji wangu wa nje ya nchi,katika maelezo yake bwana yule anadai kuwa kama mtanzania ingawaje yuko nje ya nchi ila anasikitishwa na vifo vinavyoendelea hapa nchini ambavyo kwa maelezo yake anadai ni kutokana na uzembe.
  Nikiunganisha mawazo ya ndugu yangu huyu na mfululizo wa ajali zinazoendelea kasha nenda huko mashuleni unajua huwa nashindwa kuelewa kwanini shule ziwake moto? Eti watoto wanakufa kila siku, sehemu za makazini ndio usiseme kabisa jinsi watu wanavyoteketea huko viwandani ajali ni nyingi tu sitaki kuongea habari za migodini hapa.
    Chukulia mfano tukio la hivi karibuni la wale wafanyakazi waliokuwa wanajenga uwanja wa uhuru walikuwa hawana hata vifaa vya kujilinda yaani “they were exposed to danger” sasa kwa muktadha huu ndio najaribu kujiuliza nchi hii haina sheria za ulinzi makazini? Au sheria zimewekwa ili zivunjwe? Waziri mwenye dhamana anafanya nini? Watu wanakufa kila uchao, halafu fidia zenyewe ndio hivyo tena badala ya kuwapooza wahanga zinazua malalamiko kwa jinsi wanavyopunjwa. Naam! Taifa letu halilindi watu wake wanataka nani afanye? Je tukifa wote hao viongozi watamwongoza nani? Au kutawala nini? Labda makaburi yetu..Tafakari!

1 comment:

Goodman Manyanya Phiri said...

Kama ni hivyo kweli, aiseee!! Poleni sana, Ndugu zetu Watanzania!!!