Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, April 10, 2011

Breaking News......Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Secretariti yake Yavunjwa usiku huu Mjini Dodoma

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi(CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete amevunja kamati kuu pamoja na secretarieti ya chama hicho inayo ongozwa na katibu mkuu Yusuph Makamba.
Hatua hiyo imechukuliwa na mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kutokana na hali ya chama hicho kuwa mbaya katika swala zima la utendaji.
Hata hivyo aipo tafutwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Yusuph Makamba, Hakutaka Kuzungumzia Lolote zaidi ya kusema Kwamba "Huu ni wakati wa kulala na si wakati wakuzungumzia swala lolote"
Habari kwa Hisani ya Michuzi

1 comment:

Anonymous said...

Ni muhimu sana hilo kwa sababu chama kimeondoka kwenye misingi imara iliyowekwa na waasisi,imejikita zaidi na wafanyabiashara na viongozi wenyewe kuwa wafanyabiashara na si kuwatumikia wananchi. Chama hakisimamii ipasavyo serikali kwa ajili ya kuoneana haya,huduma za mahakama,polisi na vyombo vya sheria havitendi haki tena kwa mwananchi wa kawaida ilhali viongozi wa chama wakiangalia uwozo serikalini bila kuukemea. UMOJA WA VIJANA PIA UONGOZI WOTE UONDOKE NA NI BUSARA ZAIDI VIONGOZI KUZUIA WATOTO WAO KUGOMBEA UONGOZI MAANA KUNA HISIA FULANI ZINAJENGEKA KWENYE JAMII