Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, March 15, 2011

Mdau anaomba Ushauri kwa kilicho tokea kwa Ndugu yake...

Kilio Changu...
Dear Mbeyayetu blogg,
Mimi ni msomaji wako wa kila siku, bali leo naomba kwa mala ya kwanza unipeperushie mahuzuniko yangu kwenye blogg yetu.Lengo likiwa vyombo vya dola vifuatilie haki na labda liwe fundisho kwa  waTanzania wezangu.Jumatatu tarehe 18, Oktoba 2010, pale stendi ya magari mizigo-Uyole, Mbeya.Shemeji yangu,dereva Leopard Josephat alipigwa sana mpaka akafariki na watu watano wanaoujulikana kama maafisa ukusanyaji ushuru.Kisa kikiwa hajalipa ushuru wa shilingi 500 wa gari.  Leopard ameacha mke na watoto wawili.Je nani atawaleya?Je nihaki ya kumpiga mtu mpaka anakufa kwa kosa lolote lile?  Je uhai wa mtu ni bei ghani?Je waTanzania ubinadamu  umekwisha ya kwamba tunaweza kutoa roho ya mtu na kusababisha huzuni na majonzi mengi kwenye familia?  Naandika kwa majonzi mengi ya kumpoteza ndugu yangu, lakini si kwa moyo wa kisasi nikitegemea vyombo vya sheria vinafuatilia ili haki itendeke.  Namalizia kwa kusema Kiongozi mpenda haki, Martin Luther King, alisema, kama haki haipatikani sehemu, basi ni tishio kwa sehemu zote zote zenye haki- ("injustice anywhere is a threat to justice everywhere").  
Mimi naitwa Kocha Somola toka Chicago, USA.  Asante.

1 comment:

Anonymous said...

Nakukubali wewe kweli sauti yetu sisi wana Mbeya popote tulipo duniani. Kocha Somola-Asante.