Zoezi la utoaji wa Kili Tanzania Music Awards lilipomalizika hapo juzi pale Diamond Jubilee Hall jijini Dar-es-salaam,jina moja lilibakia katika vinywa na bongo za mashabiki wa muziki na wote waliofuatilia tuzo hizo.Jina hilo sio lingine bali la Abbas Hamisi au maarufu kama kwa jina la kisanii la 20%.
Kijana huyo mzaliwa wa mkoa wa Pwani ambaye unaweza kusema bado ni msanii asiyejulikana sana hususani nje ya mipaka ya Tanzania,aliibuka “Mfalme” kwa kutwaa jumla ya tuzo 5 miongoni mwa vipengele 7 alivyokuwa ameteuliwa katika kuwania tuzo hizo. Kwa ujumla 20% aliibuka mshindi kama Male Artist of The Year(Msanii Bora wa Kiume), Best Male Singer(Mwimbaji Bora wa Kiume), Best Song Writer of The Year(Mwandishi Bora wa Nyimbo wa Mwaka) na huku kibao chake cha Tamaa Mbaya kikiibuka mshindi katika kipengele cha Best Song of The Year(Wimbo Bora wa Mwaka) na Ya Nini Malumbano kikiibuka mshindi katika Best Afro Pop Song(Wimbo Bora wa Afro Pop).
Kusoma zaidi Bofya hapa..Bongo Celebrity
No comments:
Post a Comment