MWENYEKITI wa Soko la Sowetojijini Mbeya, Honola
Mbogella, amefikishwakatika mahakama ya Mwanzo Mbeya mjinikwa tuhuma za
kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.
Kufuatia kukamatwa
kwaMwenyekiti huyo kulisababisha zaidi yawafanyabiashara 1000 wanaondesha
shughuli zao za kibiashara katika masokomatano yaliyopo Jijini Mbeya,
kuandamana na kuizunguka mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, wakishinikiza
mahakama hiyo kumuachia huru.
Mwenyekiti huyo,amefikishwa katika
mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, leo na kesi yake kusikilizwa majira ya saa
tatu asubuhi ambapo kesi hiyo ilivuta hisia za watukutokana na kundi hilo
la wafanyabiashara kuizunguka mahakama hiyo, huku jeshila polisi likilazimika
kuimarisha ulinzi.
Akisomewa mashitaka hayo Mbele ya Hakimu wa Mahakama
ya mwanzo ya Mbeya MjiniUbaswege Mathew, karani wa Mahakama hiyo, Sioni
Kasunga, alisema mtuhumiwa huyoalifanya kosa hilo January 10 mwaka huu akiwa
katika eneo lake la kazi la Sokola
Soweto lililopo Jijini Mbeya. Alisema, kwa mujibu wa kifungu kidogocha cha sheria namba 101(a) sura ya 288iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mtuhumiwa aliwazuia watumishi wa umma wahalmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya kazi yao ya kukusanya ushuru.
Soweto lililopo Jijini Mbeya. Alisema, kwa mujibu wa kifungu kidogocha cha sheria namba 101(a) sura ya 288iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mtuhumiwa aliwazuia watumishi wa umma wahalmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya kazi yao ya kukusanya ushuru.
Alisema, mtuhumiwa aliwazuiawafanyabiashara
hao kugoma kutozwaushuru wa shilingi 200 hadi 300 na halmashauri ya Jiji
la Mbeya kwa maelezokwamba licha ya wafanyabiashara hao kulipiatozo hiyo
kwa kipindi kirefu bado soko hilo limeendelea kukithiri kwa uchafu.
Aidha,
kutokana na kosa hilo,Hakimu wa mahakama hiyo, Ubaswege Mathew,baada ya
kusikiliza maelezo hayo,alitoanafasi kwa mtuhumiwa ambaye alikana shitaka hilo
hivyo, hakimu kuhairisha kesi hiyo mpaka kesho na kwamba dhamana kwa
mtuhumiwa ipo wazi.
“Kesi hii nimeihairisha mpaka kesho
asubuhi, mtuhumiwa anahaki ya kuwekewadhamana kwa masharti ya kiasi cha fedha
cha shilingi milioni mbili na wadhaminiwawili mmoja akiwa ni mtumishi wa
serikali,”alisema Wakati kesi hiyo ikiendeleamahakamani hapo, umati mkubwa wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zaokatika masoko matano ya Soweto,Uyole, Mabatini, Sokomatola na Uhindiniulijitokeza na kuizunguka mahakama hiyo kwa kile walichokidai kwamba Mwenyekityi huyo ameonewa.
serikali,”alisema Wakati kesi hiyo ikiendeleamahakamani hapo, umati mkubwa wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zaokatika masoko matano ya Soweto,Uyole, Mabatini, Sokomatola na Uhindiniulijitokeza na kuizunguka mahakama hiyo kwa kile walichokidai kwamba Mwenyekityi huyo ameonewa.
Wakizungumza naMbeya yetu ,nje ya mahakama, wafanyabiashara hao
ambao waligoma kutaja majina yao, walisemawao wamegoma kulipa ushuru huo
kutokana na halmashauri kushindwa kuetekelezamajukumu yao ya ukarabati wa
miundombinu pamoja na usafi wa mazingira hivyoMwenyekiti huyo hausiki na
suala lakuwashawishi kugoma kama inavyodaiwa na halmashauri.
Hata
hivyo, wafanyabiashara haowamegoma kuendelea na shughuli zao mpaka suala hilo
litakapo patiwa ufumbuzikwa halmashauri kurekebisha miundombinu na usafi wa
mazingira katika maeneo yabiashara.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
2 comments:
Wamefanya vema sana wafanyabiashara kuandamana. Usafi ni jambo la msingi sana na daima maandamano huleta maendeleo na mabadiliko sehemu nying. Well done.
Kwa hatua ya uongozi wa jiji kuchukua hatua za kumshitaki kiongozi wa soko kutokana na madaiya uchafu uliokithiri sokoni hapo ni ukandamizaji uliokithiri na usiovumilika haswa ukizingatia ushuru wa sokoni sokoni hulipwa na wahusika ikiwa ni sehemu ya gharama za uendeshaji wa soko hilo ikijumuisha usafi unaofanywa na halmashauri. ninadhani imefika mahali mheshimiwa Rais Kama meuzi wa nafasi hizi kuangalia upya wateule wake na chama pia kuangalia upya madiwani na mameya wasijua wajibu wao, na namna wanavyopokea maoni ya wananchi na wadau mbalimbali.
Post a Comment