Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, |
Waliofariki katika ajali ya gari
iliyokuwa ikisafirisha maiti na kupinduka kisha kusababisha vifo vya watu
watano wamefahamika majina yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,
Ahmed Msangi, alithibitisha kujulikana kwa majina hayo na kuwataja kuwa ni
wanawake watatu na wanaume wawili ambao ni Sophia Omary mkazi wa Mbalizi, Stela
Mwaluswaswa Mkazi wa Tunduma na Suzana Melele mkazi wa Mbalizi Mkoani Mbeya.
Aliwataja marehemu wengine kuwa ni wanaume
waliotambuliwa kwa Bulele Mwaipaja(48) mkazi wa Uyole jijini Mbeya na
Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Mbozi Misheni aliyetambulika kwa jina la Jacob
Nyaluke(17).
Alisema kati ya majeruhi wa
ajali hiyo Wanaume ni 16 na Wanawake 16 hivyo kufanya idadi yake kufikia 32kati
yao ambao wamelazwa katika Hospitali za misheni Igogwe na Makandana – Tukuyu.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni
hitilafu katika mfumo wa breki wa gari hilo ambapo dereva aliyefahamika kwa
jina la Robert Mwakibibi (37) mkazi wa Uyole kuacha njia na kasha kupinduka katika Kijiji cha Kantela Wilayani Rungwe Mkoa wa mbeya.
Aliongeza kuwa ajali hiyo ilitokea
jana majira ya saa 11:45 asubuhi huko katika kijiji cha Kantela-Ntokela, kata
ya Ntokela, tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya katika barabara
kuu ya Mbeya/Tukuyu ambapo Dereva alikimbia mara baada ya tukio na juhudi za
kumtafuta zinaendelea.
Mwisho.
|
1 comment:
Gari aina gani, namba za usajili. Jina la dereva. Gari ilitokea wapi na ilikuwa inaelekea wapi. Habari ikamilike mwanahabari.
Post a Comment