Askofu wa Jimbo
wa Jimbo la Kusuni Magharibi, Alinikisa Cheyo,
SINTOFAHAMU
ya mwisho wa mgogoro unaondelea ndani ya Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la
Kusini Magharibi imeendelea kuwakumba waumini wa kanisa hilo licha ya Kamati ya
Ulinzi na usalama ya Mkoa kuagiza litafutiwe ufumbuzi wa haraka.
Hali
hiyo imeonekana kushindwa kupata muafaka baada ya Mkutano wa Halmashauri kuu ya
Jimbo kuvurugika na hatimaye kuusogeza mbele baada ya kutokea kutoelewana.
Akizungumza
na vyombo vya habari ofisini kwake , Askofu wa Jimbo wa Jimbo la Kusuni
Magharibi, Alinikisa Cheyo, wakati akitoa taarifa ya Halmashauri kuu ya Kanisa
kuhusu mgogoro katika mkutano uliofanyika Novemba 15 mwaka huu Vwawa mkoani
Mbeya alisema baada ya mkutano kuvurugika ukasogezwa mbele hadi Disemba 16, mwaka
huu utakapofanyika tena.
Askofu
Cheyo alisema mkutano huo ulifanyika baada ya kutoa tamko novemba 11, mwaka huu
la kuitisha Halmashauri kuu kufuatia mgogoro unaoendelea ndani ya kanisa hilo
na kusababisha baadhi ya waumini kufunga ofisi kwa minyororo na kusababisha
Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kuingilia kati.
Alisema
kwa mujibu wa Katiba ya kanisa aliwaagiza kamati tendaji kuwaatarifu wajumbe
wote wa halmashauri kuu ya Jimbo kuhudhuria Mkutano wa Novemba 15 mwaka huu.
Alisema
pia aliagiza katika mkutano huo barua iliyoandikwa na Mchungaji Buyaya julai
28, mwaka huu aliyoiandika ya kuomba msamaha ili halmashauri kuu irejee kwa
upya kuangalia maudhui ya barua hiyo na kutafuta uwezekano wa kumaliza mgogoro
huo kwa nia ya kusameheana.
Alisema
kamati tendaji ilitekeleza kile alichokiagiza isipokuwa barua ya Mchungaji Buya
kwa madai kuwa hawakuona sababu ya kuleta barua hiyo kwa sababu Askofu alitoa
tamko la kuitisha mkutano huo kinyume cha Katiba ya Kanisa sehemu ya V ibara ya
34,b,vi ya mwaka 2012.
Alisema
kutokana na majibu hayo ndipo hali ya kutoelewana ndani ya mkutano iliapoanza
kuibuka na kuhatarisha hali ya usalama hali iliyomlazimu Askofu kujitetea kuwa
alitoa tamko kwa mujibu wa Katiba ya Moravian duniani (Church order of the
unitas fratrum chapter XIII,A,2,C of 2009) ambayo inasema Askofu ana mamlaka ya
kutamka kwa niaba ya kanisa na maoni ya askofu yanapaswa kuzingatiwa na kanisa.
Alisema
mgogoro ndani ya mkutano ulizidi kupamba moto baada ya Kamati kusisitiza
msimamo wao huku baadhi ya wajumbe wakigawanyika kuhusu kumrudisha Makamu
Mwenyekiti madarakani na wengine wakipinga wakidai hata akirudishwa atafanya
kazi katika mazingira magumu.
Aliongeza
kuwa baada ya mvutano mkali ikaamliwa Disemba 16, mwaka huu maamuzi rasmi
kuhusu mgogoro na mustakabari wa kanisa vitatolewa na Hlmashauri kuu.
Askofu
alisema kulingana na kikao hicho kuanzia sasa msemaji wa kila jambo
linaloendelea ndani ya kanisa atakuwa Makamu Mwenyekiti Mchungaji Zakaria
Sichone hadi muafaka utakapopatikana na amani kurejea ndani ya Kanisa.
Alisema
pamoja na kukubaliana maamuzi kutolewa Disemba 16, mwaka huu, pia ameona
aitishe mkutano na kamati ya ushauri ya Jimbo ili kuwaeleza hali ya Kanisa
ilivyo sasa pamoja na kukutana na kamati teule ya usuluhishi wa migogoro ya
jumuiya ya kikristo Tanzania inayoongozwa na Askofu mkuu wa KKKT, Dk. Alex
Malasusa akisaidiwa na Jaji mstaafu Agustino Ramadhani ili wafanye haraka
kuingilia kati na kusuluhisha mgogoro huo ili kuzuia uvunjifu wa amani katika
kanisa.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
2 comments:
Kuna watu wamedhamiria kabisa kulitesa kanisa. Hivi ni kwanini mtu anayejiita mchungaji aendelee kung'ang'ania cheo wakati ametakiwa atoke? Kuna maslahi gani jamani?
Kuna watu wamedhamiria kabisa kulitesa kanisa. Hivi ni kwanini mtu anayejiita mchungaji aendelee kung'ang'ania cheo wakati ametakiwa atoke? Kuna maslahi gani jamani?
Post a Comment