Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka alisema baada ya kupewa taarifa hizo aliamua kufuatilia na kumbana Mtendaji huyo kuhusu madai hayo ya Wananchi ambapo Mei 23, Mwaka huu alikiri kuhusika na kudai kuwa alipewa Laki saba pekee ambazo alizikabidhi katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji.
KATIKA Hali isiyo kuwa ya kawaida Wakazi wa Kitongoji
cha Isanzo Mtaa wa Chapwa uliopo katika Kata na Mji mdogo wa Tunduma wilaya ya
Momba Mkoani Mbeya wamefanikiwa kuzikomboa fedha zilizokuwa zimeliwa na Afisa
Mtendaji wa Mtaa huo zaidi ya Shilingi Milion 14.
Tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni
katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Chapwa katika Mji huo baada ya
baadhi ya wananchi kumtuhumu Mtendaji huyo kujipatia fedha kinyume na utaratibu
kutokana na malipo ya fidia ya eneo la Kitongoji cha Isanzo lililochukuliwa na
Mamlaka ya mapato (TRA) kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba za watumishi.
Kwa mujibu wa Wananchi waliofika katika mkutano
huo uliokuwa ukiongozwa na Diwani wa kata ya Tunduma Frank
Mwakajoka(CHADEMA) walisema chanzo cha Mtendaji huyo Daniel Sinkonde kula fedha
hizo ni kutokana na kufoji majina ya wakazi wa Kitongoji hicho waliokuwa wakistahili
kulipwa fidia kutoka TRA.
Walisema wakati Mamlaka ya Mapato ilipohitaji
majina ya wakazi hao kwa ajili ya kulipwa fidia, Mtendaji huyo aliamua kutunga
majina sita ambayo aliyapeleka TRA ambapo Mamlaka hiyo iliandika hundi kwa
wahusika ambao baada ya kukabidhiwa fedha zao walizipeleka kwa Mtendaji ambaye
aliwalipa Shilingi Laki 5 kila mmoja kama kifuta jasho.
Waliongeza kuwa baada ya kukamilisha kwa zoezi
hilo mtu mmoja kati ya Sita ambaye alijulikana kwa jina la Vasta Choka alilipwa
Shilingi laki Tatu badala ya Laki Tano kama wenzie walivyolipwa ambapo
alipojaribu kufuatilia alibaini kudhulumiwa ndipo suala hilo lilipotinga kwa
wananchi na hatimaye kumfikia Diwani.
Waliyataja majina yaliyoghushiwa na viwango vya
fedha kwenye mabano vilivyolipwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa ni Elisa
Sinkonde (mil 3,281,680/=),John Siwakwi ( Mil 2,387,800/=), Frank Mshani ( Mil
2,740,080/=), Vasta Choka 2,542,680/=), Jumatatu Silagwe (Mil 1,279,320/=) na
Ezekia Kuyokwa (Mil 1,961,400/=) na jumla yake ni Shilingi Milion 14,192,960/=.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Tunduma Frank
Mwakajoka alisema baada ya kupewa taarifa hizo aliamua kufuatilia na
kumbana Mtendaji huyo kuhusu madai hayo ya Wananchi ambapo Mei 23, Mwaka
huu alikiri kuhusika na kudai kuwa alipewa Laki saba pekee ambazo
alizikabidhi katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji.
Alisema kutokana na kukiri huko pamoja na
kurudisha fedha hizo alienda katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato na kubaini kuwa
Mtendaji huyo alikuwa ameshalipwa zaidi ya Milion 14 kutokana na malipo ya
Fidia ya viwanja kwa majina feki yaliyopelekwa.
Mwakajoka aliongeza kuwa awali Mtendaji huyo
aliahidi kuzilipa fedha zote na kwamba endapo angeshindwa aliweka nyumba yake
kama dhamana nyumba yenye hati ya kiwanja namba KAL 521 yenye thamani ya
Shilingi Milion 30.
Kutokana na kusuasua huku baadhi ya wananchi
kutojua mustakabali wa Mtendaji huyo waliamua kuitisha mkutano wa Hadhara kwa
lengo la kumshinikiza Mtendaji huyo kuzirejesha fedha zilizobaki ambapo
alipofika Mkutanoni alikutwa na Shilingi Milion 4 tu hivyo wananchi kupandwa na
hasira ya kutaka kuuza nyumba yake.
Baada ya kutokea kwa mtafaruku huo ndipo alipojitokeza
Mfanyabiashara mmoja aliyefahamika kwa jina la Adolf Mwanyangala kumdhamini kwa
kumkopesha Milion 3 na Laki tano ambazo alilipa na kufanikisha kumaliza
deni lote.
Aidha alipotakiwa kuzungumza lolote Mtendaji huyo
aliomba msamaha na kuongeza kuwa halikuwa kusudio lake na alifanya hivyo kwa
bahati mbaya tu na kuwaomba wananchi wamsamehe.
Pia wananchi walimwomba Mkurugenzi Mtendaji wa
Mji mdogo wa Tunduma kumfukuza kazi kabisa Mtumishi huyo kutokana na kutokuwa
na sifa za utmishi wa umma.
Picha na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
|
2 comments:
Safi sana wananchi sasa wamekuwa na ujasiri, wametafakari na kuchukua hatua! Diwani
Hongera nyingi sanaaa kwa Diwani na wananchi wote kwa kudhibiti dhuluma,rushwa na uizi. Nawapa pongezi kw awananchi wote wa kijiji hicho cha Tunduma, kazeni mwendo huo huo msikubali kuibiwa wala kudanganywa. hongera sana. na ninashukuru kwa blog hii kutuletea habari hiii.
Post a Comment