Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Mbeya, Benard Winga ambaye ndiye mwezeshaji wa semina akiendelea kutoa somo.
Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya ya Mbeya Rehema Matingisa akiendelea kutoa somo kwa washiriki wa semina.
Mratibu Ukimwi Wilaya ya Mbeya, Kelvin Kisoma akisisitiza jambo kwa washiriki wa Semina hiyo.
Wawezeshaji wakiangalia jambo kwenye kompyuta yao ikiwa ni kuweka sawa mikakati kabla ya kuanza semina.
Washiriki wa semina wakifuatilia kwa makini kutoka kwa wawezeshaji semina kuhusu Ukimwi Wilaya ya Mbeya.
HALMASHAURI ya Wilaya ya
Mbeya mkoani hapa inaendesha semina ya siku mbili kwa wadau wa kudhibiti Ukimwi
wilayani humo ili kufikia malengo ya Sifuri tatu.
Semina hiyo inafanyika Juni
18 na 19, Mwaka huu katika ukumbi wa kituo cha Walimu kilichopo Mbalizi Wilaya
ya Mbeya mkoani hapa.
Semina hiyo imehudhuriwa
na wadau ambao ni sekta binafsi zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi,
viongozi wa dini, Wazee, Vijana na asasi binafsi kutoka wilayani hapa.
Akizungumza kwenye
semina hiyo,Mratibu wa Ukimwi Wilaya ya Mbeya, Kelvin Kisoma, amesema mpango
mkakati wa mwaka uliopita wa 2007/2008 ulioishia 2011/2012 umeonesha mafanikio
makubwa kutokana na kupungua kwa maambukizi mapya ya Virusi vya ukimwi kwa
asilimia 4 jambo linaloonesha mafanikio kuelekea sifuri tatu.
Amesema katika kipindi
hicho kulikuwa na maambukizi ya asilimia 13 lakini baada ya kuanza utekelezaji wa
mpango huo wa sifuri tatu imefikia asilimia 9 ambazo ni malengo yao kuwa
zitapungua katika mpango wa miaka mitano ijayo.
Kwa upande wake mmoja wa
wawezeshaji wa Semina hiyo ambaye pia ni Mratibu Msaidizi wa Ukimwi Wilaya ya
Mbeya, Edah Misana, ameongeza kuwa katika mpango mkakati wa miaka mitano ijayo
Halmashauri imejiwekea mikakati mbali mbali ili kuhakikisha wanafikia malengo
ya sifuri tatu ambazo ni kuhakikisha kuwa hakuna maambukizi mapya, kupunguza
unyanyapaa pamoja na vifo vinavyotokana na Ukimwi.
Ameitaja baadhi ya
mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kulenga makundi ambayo ni vijana walioko
mashuleni na wasio mashuleni, walemavu, walioko kwenye ndoa, viongozi wa dini,
wazee na watu mashuhuri.
Amesema kwa kuanzia hivi
sasa Halmashauri imefanikiwa kuanzisha klabu kumi za kudhibiti ukimwi mashuleni
kutoka kwenye kata Kumi ndani ya
Halmashauri hizo.
Kwa upande wake
Mwezeshaji wa Semina hiyo, Benard Winga ambaye pia ni Afisa Maendeleo Wilaya ya
Mbeya, amesema mafanikio ya kufikia sifuri tatu yatafanikiwa endapo jamii
itakubali kubadilika na kuitikia na kuungana na Halmashauri katika kupambana na
maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Ameongeza kuwa
Halmashauri inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika kupambana na
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambapo alizitaja baadhi kuwa ni pamoja na
baadhi ya waathirika kuacha kutumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi(ARV).
Amezitaja changamoto
zingine kuwa ni pamoja na mgongano wa kiimani juu ya matumizi sahihi ya kinga
zikiwemo Kondomu kuwa baadhi ya dini imani zao zinapinga pamoja na wataalamu wa
tiba asili kutoa tiba za ukimwi bila kuzingatia vipimo sahihi.
Na Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment