Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, August 31, 2012

WATANO WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMFANYIA FUJO DC MBARALI MBEYA


SAKATA la MKUU wa Wilaya ya Mbarali Gulamu Hussen Kiffu  kunusurika kuumizwa na wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Chimala kilichopo Wilayani humo mkoani Mbeya baada ya kuvamia gari lake na kuvunja vioo,kutoa upepo wa matairi  kutokana na Serikali kufunga chuo hicho kwa kutokuwa na hadhi ya kudaili wanafunzi, watu watano wamefikishwa mahakamani.

Kutokana na vurugu hizo zilizotokea chuoni hapo jana jioni, Jeshi  la polisi Mkoani Mbeya linawashikilia wanafunzi  sita    akiwemo Mkuu wa Chuo  hicho  Francis Mtega  kwa  tuhuma za kuhamasisha vurugu  zilizopelekea  kuharibu gari la Mkuu wa Wilaya ya  Mbarali. 

Kamanda wa polisi Mkoani hapa Diwani Athuman  alisema  baada ya mkuu wa wilaya kuongozana na baadhi ya viongozi wa serikali  hususani kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwa lengo la kutaka kujua sababu za chuo hicho kuendelea kufundisha wakati serikali ilitoa agizo kifungwe ndipo hapo walipovamiwa na wanachuo hao.

Alisema   tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya kuwasili Chuoni hapo kwa  lengo la  kuzungumza na uongozi wa chuo ndipo baadhi ya wanafunzi  walivamia gari la Mkuu wa Wilaya na kuanza kuvunja vioo kwa kutumia mawena kisha kutoa upepo kwa malengo yasiyojulikana.

Kamanda Athumani alisema tukio hilo linaonesha ni mpango uliokuwa umepangwa na uongozi wa Chuo  kwa muda mrefu kwani serikali ina malengo mazuri kwa watanzania  na lengo kuu ilitaka chuo hicho kisajiliwe  ili kitambulike  na Serikali na kuweza kutoa wauguzi walio na sifa na kuwawezesha kupata ajira itakayotambulika serikalini. 

Aliongeza kuwa  kitu cha kushangaza ni madaraka aliyonayo mkuu wa chuo hicho ambapo yeye mwenyewe ni mwalimu na mhasibu na kwamba kulikuwa hakuna sababu ya kufanya vurugu bali  kilikuwa ni kitu cha kutoa vielelezo vya udaili wa chuo.

Alisema katika uchunguzi wa awali  umebaini kuwa chuo hicho kimeanza muda mrefu na tayari  kimeweza kutoa wauguzi katika Nyanja mbalimbali  bila ya serikali kutambua  kama hakijasajiliwa na hakitambuliki.

Kwa hisani ya Venance Matinya, Mbeya.


Thursday, August 30, 2012

WALIOGOMA KUHESABIWA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI – MBEYA


 Pichani wananchi waliokataa kuhesabiwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bwana Guram Hussein Kifu. katikati ni Kiongozi wa Mgomo Bwana Ally Mwangoto, kutoka dini ya Kiislamu wanaojiita wenye msimamo mkali wakiwa chini ya ulinzi katika mahabusu ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,wakisubiri kupelekwa Polisi wilayani humo.

Licha ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka waislamu  nchini kushiriki zoezi la Sensa  ya watu makazi, hali hiyo imeonekana kuwa tatizo kwa kijiji cha Ruiwa Kata ya Ruiwa Wilayani Mbarali  ambapo watu wasita wanaosadikiwa kuwa ni waislamu  wenye msimamo mkali kugoma kuhesabiwa  kwa madai  kuwa serikali imepuuza  madai yao.

Imeelezwa kuwa waislamu hao walishaeleza serikali kuwa hawako tayari kuhesabiswa lakini bado serikali imeshindwa kutekeleza matakwa yao na hivyo kukataa kuhesabiwa.

Akizungumza na gazeti hili jana kuhusiana na madai hayo , Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa Bw. Jordan Masweve alisema kuwa kwa kata zoezi la sense toka limeanza imekuwa ni tatizo kubwa sana kutokana na watu hao kuonyesha msimamo wao wa kutotaka kuhesabiwa.

“Wao wanadai kuwa hawapo tayari kuhesabiwa hata iweje msimamo wao ni mmoja hata wafanywe nini lakini suala ni kutokubali kuhesabiwa tu kwa madai serikali imeepuza madai yao toka mwanzo ya kutotaka kuhesabiwa”alisema.

Bw. Masweve alisema tukio hilo limetokea  Agosti 27 mwaka huu majira ya saa 8.30 mchana  katika kijiji cha Ruiwa wakati makarani wa sense  walipofika katika makazi wa wananchi hao  wakiongozwa na Mtendaji wa kijiji  kwa lengo la kuwataka wakubali kuhesabiwa lakini waligoma.

Alisema  hata hivyo zilifanyika jitiha za kuwasihi kushiriki zoezi hilo  lakini hawakutaka kukubali  ndipo mgambo wa kijiji walipowakamata na kuwapeleka kwenye ofisi ya Kata.

Bw. Masweve aliwataja waislamu waliokamatwa kuwa ni Ally Mwangoto,Subeti Juma, Abinala, Pembe ,Ally Suleiman pamoja na Nawab Suleiman licha ya kufikishwa katika ofisi ya kata bado waliendelea kuwa na msimamo wao  kuwa hawako tayari kuhesabiwa na kudai kuwa vyovyote itakavyokuwea wapo tayari  hata kuchinjwa au kufungwa jela lakini si kuhesabiwa.

Hata hivyo alisema kuwa waislamu hao walidai kuwa hata Mkuu wa Wilaya akifika hapo hawako tayari kuhesabiwa msimamo wao ni mmoja tu .

“Bado tupo nao hapa ofisini tukisubiri Mkuu wa Wilaya ya Mbarali ,na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbarali ili waje kuwachukua  watu hawa”alisema.

Aidha aliongeza kuwa kabla ya zoezi hilo kuanza  kulikuwa na mikutano ya  hadhara ambayo ulikuwa unaendeshwa na  viongozi wa kiislamu kutoka Jijini Mbeya  walikuwa wakihamasisha waislamu wenzao kuwa ambao hawatakuwa tayari kushiriki zoezi hilo kukimbilia misikitini ambako watawapelekea chakula mpaka zoezi hilo litakapokuwa limekamilika.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kuelekea kijiji cha Ruiwa  Mkuu wa Wilaya Mbarali Bw. Gulamu Hussen Kiffu alisema amepata taarifa za tukio hilo lakini bado hajafika huko lakini yupo njiani kuelekea huko ili aweze kujua undani wa tukio hilo.

“Kwasasa nipo kwenye gari naelekea Ruiwa kwa ajili ya tukio hilo mara baada ya kufika na kuangalia tukio lilivyo nitatoa taarifa kamili na hatua zipi ambazo tutakuwa tumechukua”alisema.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Bw.Athuman Diwani alisema bado hajapata taarifa hizo na kudai kuwa taarifa zote za matokeo atatotoa mara baada ya zoezi la sense kumalizika.

Picha na Habari na Ezekiel Kamanga,Mbarali.

Wednesday, August 29, 2012

KUKOSEKANA KWA OFISI ZA SHIRIKA LA VIWANGO (TBS) MBEYA VIWANDA VIDOGODOGO VYA KUSINDIKA CHAKULA NA MAFUTA YA KULA HAVIJAWAHI KUKAGULIWA WALA KUJUWA UBORA WAKE KWA WALAJI

Muuza mafuta ya alizeti maeneo ya soko la sido Mwanjelwa Mbeya akiendelea kujaza mafuta ya alizeti kwenye mageroni ya lita tano na moja toka mojakwamoja kwenye kiwanda bila ya kukaguliwa wala kujua ubora wake kwa mlaji 
Mama huyu kamera yetu ilimnasa akizoa mabaki ya mafuta toka kwenye mapipa  kiwandani hapo
Hii ndiyo hali halisi ya viwanda vyakukamulia mafuta ya alizeti jijini Mbeya tunaimani wahusika wa afya mpo na mnaliona hili
Mama huyu muuza mafuta ya alizeti akitoa karatasi ya nembo ya maji ya rungwe ili mlaji asijue kuwa chupa hiyo ilitumika kuhifadhia maji je usafi wa kusafisha chupa hizo husimamiwa na nani? maana chupa nyingi huokotwa mitaani na majalalani
Mama Asha moja ya wamiliki wa mashine za kukamua mafuta aina ya alizeti Mbeya yetu ilipomuuliza je ameshawahi kukaguliwa ubora wa mafuta anayokamua kwenye kiwanda chake  amesema hajawahi tangu aanze biasharayake hiyo zaidi ya miezi sita iliyopita 
Hii bidhaa baadhi ya kina mama wameilalamkia haina ubora na inawatoa vidonda hatujapenda kutoa picha za akina mama hao walioleta ila zipo na kila mhusika tukimuuliza anasema watu wa viwango ndiyo wanahusika sasa mbeya hakuna ofisi za viwango je wafanyeje akina mama hao waliopata matatizo?
Afisa mamlaka ya chakula na dawa mbeya tulipomuuliza juu ya swala hili la hifadhi ya  wanawake yaani always alisema ofisi yake haiusiki na kukagua bidhaa hizo badalayake akatueleza tuende ofisi za TBS yaani shirika la viwango  ambalo nalo Mbeya hawana ofisi wala mwakilishi yaani sasa tumebaki hewani na kujiuliza sasa nani muhusika?

Tuesday, August 28, 2012

LILE SAKATA LA WACHINA KUVAMIA KIWANJA NA KUANZA KUCHIMBA UDONGO KATA YA ILOMBA JIJINI MBEYA HILI HAPA

Kenneth Mwang’amba ambaye ndiye anayedai kulimiliki eneo la kiwanja hicho chenye hati miliki yenye namba 2459, Ilomba alisema kitendo walichofanya wachina hao kufanya shughuli za uchimbaji katika eneo  lake ni ukiukwaji wa sheria.

Akiwa na mwanausalama akipelekwa katika kituo cha polisi  maana bwana Kenneth aliamua kujitoa muhanga jana kuwa katapira limmalize katika kiwanja chake 

Bwana Kenneth viatu aliviona vizito wakati wa sakata hilo na wachina

Msemaji wa Skauti Mkoa wa Mbeya Uswege Kagubo Mwaitebele ambaye pia ni mkufunzi wa Skauti alisema waliwaruhusu wachina kuchimba eneo hilo kwa makubaliano ya kuwajengea  kituo cha kufundishia skauti hivyo hawakuona sababu za kusubiri.Afisa ardhi wa Jiji la Mbeya Ephraimu Mkumbo  alikiri kuwepo kwa mgogoro wa eneo hilo huku akiwatupia lawama Skauti  kwa kufanya shughuli zao kinyume na taratibu ambapo alisema wameshindwa kuonesha hata ofisi zao zilipo kwa ajili ya ufuatiliaji wa madai hayo.

Hii ndiyo hali halisi ya ya kiwanja hicho


Hii ndiyo barabara inayojazwa udongo huo


Mchina katulia anasubiri oda ya chakula toka kwa mama ntilie wala hana wasiwasi na mgogoro huo


KAMPUNI  ya wachina inayoendelea na  ujenzi wa barabara za Jiji la Mbeya  ( CICO), imedaiwa kuvamia eneo la  wananchi  na kuanza kuchimba vifusi vya udongo kinyume cha taratibu katika eneo la Machinjioni Kata ya Ilomba.

Imeelezwa kuwa Kampuni hiyo, imeingizwa mjini na watu wanaojitambulisha kwamba wao ni wamiliki  halali wa ardhi hiyo hivyo kuingia mkataba feki ambao umesababisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa na mmiliki halisi wa eneo hilo.


Kitendo cha kampuni hiyo kuingia kwenye ardhi hiyo na kuanza kufanya kazi kilipelekea wakazi wa eneo hilo kufanya vurugu zilizoambatana na kupiga mawe mitambo na magari  ya wachina hao.
  
Akizungumza na Mbeya yetu Kenneth Mwang’amba ambaye ndiye anayedai kulimiliki eneo la kiwanja hicho chenye hati miliki yenye namba 2459, alisema kitendo walichofanya wachina hao kufanya shughuli za uchimbaji katika eneo  lake ni ukiukwaji wa sheria.

“Hili eneo mimi nalimiliki kihalali licha ya kuwepo kwa  mgogoro na skauti ambao awali walinyang’anywa eneo hili baada ya kushindwa kutimiza baadhi ya vigezo na kukabidhiwa kwangu,”alisema


Mwang’amba alisema eneo hilo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati yake na Skauti Mkoa wa Mbeya ambao walivamia eneo hilo bila kufuata taratibu huku mamlaka zinazohusika zimeshindwa kutoa ufafanuzi kuhusu nani ndiye mmiliki halali wa eneo hilo.

Alisema baada ya kukosa maelewano na skauti, Halmashauri ya Jiji iliamua eneo hilo lichukuliwe na Skauti ambapo pia walitakiwa kulipa fidia kwake baada ya makubaliano kutokana na uharibifu uliokuwa umetokana.

Aliongeza kuwa kutokana na Skauti kushindwa kulipa fidia hivyo hawakuwa na uhalali wowote wa kuendesha shughuli ya aina yoyote katika eneo hilo kutokana na Skauti kushindwa kulipa fedha walizokuwa wakidaiwa.

“ Kisheria hawa watu wa Skauti hawakutakiwa kufanya shughuli zozote katika kiwanja hiki kwa sababu mimi ndiye mmiliki halali wa eneo hili hadi hapo watakapokuwa wametimiza masharti hata kunilipa fidia kwa sababu awali kulikuwa na tofali ambazo ziliharibika kutokana na mgogoro ” Alisema.

Kwa upande wake Msemaji wa Skauti Mkoa wa Mbeya Uswege Kagubo Mwaitebele ambaye pia ni mkufunzi wa Skauti alisema waliwaruhusu wachina kuchimba eneo hilo kwa makubaliano ya kuwajengea  kituo cha kufundishia skauti hivyo hawakuona sababu za kusubiri.

Kuhusu mgogoro uliopo kati ya Skauti na Mwang’amba, Mwaitebele alikiri kuwepo kwa mgogoro huo ambapo naye alisema eneo hilo linamilikiwa kihalali ingawa walishindwa kulipia fidia kama walivyokubaliana.

Pia alikiri kutofuata taratibu za kuruhusu uchimbaji wa vifusi pasipokuwa na kibali kutoka katika Halmashauri husika ambapo yeye alifanya hivyo bila kuwahusisha viongozi wenzie wa Skauti kwa madai kuwa  yeye ni kiongozi wa Skauti wa kanda hivyo kama kanda haina ofisi nayeye amekuwa akijitolea kuhifadhi nyaraka za Skauti katika Ofisi yake.

Naye Afisa ardhi wa Jiji la Mbeya Ephraimu Mkumbo  alikiri kuwepo kwa mgogoro wa eneo hilo huku akiwatupia lawama Skauti  kwa kufanya shughuli zao kinyume na taratibu ambapo alisema wameshindwa kuonesha hata ofisi zao zilipo kwa ajili ya ufuatiliaji wa madai hayo.

Mkumbo alisema Halmashauri ya Jiji iliwaamuru Skauti kulipa fidia za eneo hilo kwa mhusika kama watahitaji kulimiliki kihalali ambapo alisema wamekuwa wakipiga chenga bila taarifa zozote hadi leo unapoibuka mgogoro mwingine.

“Ukweli ni kwamba mpaka sasa mmiliki halali wa eneo hili na Keneth Mwang’amba hivyo wachina hao wanapaswa kuondoka na kusitisha shughuli zao,”alisema

Hata hivyo, Kiongozi huyo alishangazwa na kitendo cha wachina hao kuchimba  vifusi katika eneo hilo  kwani walishapangiwa eneo la kuchimba vifusi eneo la  Kawetere nje kidogo ya Jiji la Mbeya hivyo wamekiuka sheria na wanachofanya sasa ni uharibifu wa Mazingira.

Monday, August 27, 2012

SHEIKH ABADILI MSIMAMO KUPINGA SENSA WAISLAMU WATAHARUKI MSIMAMO WAKE, ALIKUWA AKIHUBIRI KUPINGA SENSA MWEZI MZIMA WA RAMADHANI


SHEIKH ABADILI MSIMAMO KUPINGA SENSA WAISLAMU WATAHARUKI MSIMAMO WAKE, ALIKUWA AKIHUBIRI KUPINGA SENSA MWEZI MZIMA WA RAMADHANI MBEYA

LIVEE WACHINA WAVAMIA KIWANJA NA KUANZA KUCHIMBA KIFUSI JIJINI MBEYA

Moja ya kijiko kilichosimamishwa na wananchi wenye hasira kali kata ya ilomba jirani ya machinjio ya wanyama eneo hilo hujulikana sana kama veta limevamiwa na wachina wajenzi wa barabara za jijini mbeya kwakuchimba kifusi na kukiweka katika barabara wanazozijenga 

Hii ndiyo hali halisi wanayoifanya wachina hao
wachina hao walikuwa hawataki kabisa kubigwa picha na mwandishi wetu ila wenyewe walikuwa wanampiga picha mwandishi wetu Joseph Mwaisango

Polisi wakiwasikiliza  na kuwatuliza wananchi waeneo hilo la ilomba

Hivi ni viatu vya jamaa anayemiliki kiwanja hicho picha yake mtaiona kesho maana ilikuwa hatari sana habari kamili tutawaletea kesho baada ya kufwatilia kwa wahusika wa Ardhi jiji la mbeya

Huyu bwana ni kiongozi wa skauti Mbeya ndiyo inadaiwa kuwa ndiyo chanzo cha yote mpaka tunatoka eneo la tukio hali ilikuwa shwali kabisa baada ya wanausalama fufika na kuondaka na wahusika habari zote za tukiozima la leo tutawaletea hapo kesho baada kupata ufafanuzi mzima juu ya swala hili

MCT YATOA DOZI YA AZIMIO LA DAR ES SALAAM-MBEYA

WAWEZESHAJI WA DEFIR WAKIWA MEZA MOJA KATIKA WARSHA HIYO ILIYOFANA KUTOKA MCT NA ILIFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MTENDA SUN SET CENTRE


MWANDISHI WA MBEYA YETU JOSEPH MWAISANGO AKIWA NA WAANDISHI WENZAKE WAKIWA MAKINI KUWASIKILIZA WAWEZESHAJI WA MCT

MSHIRIKI WA WARSHA HIYO GORDON KALULUNGA AKIWA NDANI YA CHUMBA CHA WARSHA NA WASHIRIKI WENGINE AMBAO NI WAANDISHI WA HABARI WA MKOANI MBEYA.WAANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA WALIOSHIRIKI WARSHA HIYO YA DEFIR WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAWEZESHAJI KUTOKA MCT AMBAPO WARSHA HIYO ILIANZA AGOSTI 23, 2012 NA KUISHA AGOSTI 25,2012.


BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limetoa mafunzo na kuwaelimisha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya umuhimu wa Azimio la Dar es Salaam kuhusu uhuru na uwajibikaji wa vyombo vya habari (DEFIR).

Katika warsha iliyohudhuriwa na waandishi wa mkoa huo kwa siku tatu iliyofanyika katika ukumbi wa Mtenda Sunset Centre, wawezeshaji wa warsha hiyo Beda Msimbe na David Mbulumi, walitoa ufafanuzi kuhusu changamoto na Mtanziko wa maadili ya Uandishi wa Habari ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha waandishi kubaini habari zinazokiuka maadili kwenye Magazeti.

Mwezeshaji Beda Msimbe alisema kuwa kumetokea mmomonyoko wa maadili na kupoteza uzalendo kwa baadhi ya Wahariri na waandishi wao jambo ambalo linasababishwa na sababu mbalimbali ambazo aliwaachia washiriki kuzitaja ambapo baadhi ya waandishi walisema kuwa baadhi ya wahariri wamekuwa wakiwaomba rushwa waandishi wao huku hawawalipi malipo ya habari zao.

Msimbe alifundisha dhana na Misingi ya DEFIR pamoja na madhumuni yake ambapo alikumbusha wajibu na changamoto zilizoainishwa kwenye azimio hilo kwa Wamiliki wa vyombo vya habari, Wahariri, waandishi, Dola, watoa matangazo, wafadhili, wanasiasa, Mabalozi na wadau wengine wa habari.

Sanjari na hayo wawezeshaji hao walisema kuwa ni muhimu waandishi wa habari wakawa  na uzalendo badala ya kuandika habari za kuwatumikia watu wachache na kuuacha umma wa watanzania ambao ndiyo unawategemea kupata habari za uhakika ambazo hazijatiwa chumvi.

Katika warsha hiyo waandishi walioshiriki walijifunza tofauti ya uandishi wa Udaku na unaowajibika kwa jamii, uandishi wa Habari kitaaluma dhidi ya uandishi wa Media jamii mfano mitandao ya kijamii ambayo mingine haimilikiwi na watu wenye taaluma ya Habari.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya Christopher Nyenyembe, alisema kuwa warsha hiyo ni chachu mpya kwa waandishi wa habari ambao ni kioo cha jamii ambapo kutokana na warsha hiyo anaamini kuwa waandishi wamejifunza na kuelewa vema makosa ambayo walikuwa wakiyafanya awali na  kutoitendea haki jamii kwenye habari zao.


Saturday, August 25, 2012

SENSA YA WATU NA MAKAZI YAMWACHISHA KAZI SHEKH WA WILAYA YA MBARALI MKOANI MBEYA


SHEKH Yassin Bambala wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya amevuliwa wadhifa huo kwa kosa la kuhamasisha waumini wa dini ya Kiislam kususia zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalo anza usiku wa kuamkia Agosti 26,2012 kote nchini Tanzania.

Tamko hilo la kumvua wadhifa huo limetolewa na Katibu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Mbeya Shekh Juma Kila katika ofisi ya Bakwata iliyopo eneo la Sokomatola Jijini Mbeya mara baada ya kukamilika kwa maamuzi ya baraza hilo.

Katibu huyo alisema hatua hiyo imetokana na  Sheikh Bambala kushiriki na kuhudhuria vikao vya baadhi ya waislamu wanaopinga zoezi la Sensa  kufanyika kwa kuwataka waislamu wasijitokeze kuhesabiwa.

Alisema baraza hilo limebaini kuwa wapo baadhi ya viongozi wenzao ambao walikuwa wakionekana kufanya kampeni za chini chini kuungana na taasisi nyingine kuwataka waislam wasishiriki Sensa ya mwaka huu.

Alisema kitendo hicho kinapingana na msimamo wa BAKWATA na kiongozi mkuu wa Waislamu (Mufti), kuhusu kuhakikisha waislamu wanashiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.

Killa alisema wahusika hawa wamekiuka maagizo ya pamoja ya waislamu kwani awali  masheikh wa ngazi za wilaya na wale wa mikoa nchini, waliitwa na Mufti mjini Dodoma kwenye kikao cha Tume ya dini na kupeana  msimamo wa pamoja kuhusiana na zoezi la Sensa na wakakubali kurudi kwenye maeneo  kuwahamasisha waislamu wenzao juu ya umuhimu wa Sensa.

Aliongeza kuwa  wamebaini kuwa baadhi ya Masheikh, akiwemo Sheikh Bambala baada ya kurudi kutoka Dodoma, wameanza kufanya kazi tofauti na makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa.

Katibu huyo wa BAKWATA mkoa, alisema kufuatia hali hiyo wameanza kuchukua hatua kali kwa viongozi waliodhihirika na ushahidi kupatikana kuwa wamekuwa wakienda kinyume na maagizo ya Tume ya Dini hiyo.
  
Hata hivyo alisema nia  ya kumvua madaraka kiongozi huyo ni kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi wa dini hiyo ya Kiislamu anayeamua kwa matakwa yake kupingana na misimamo ya Baraza pamoja na ile ya serikali.

Aidha aliwasihi wananchi kujitokeza katika zoezi hilo na kuwapuuza baadhi ya watu wanaopita kuhamasisha ili kususia zoezi hilo.

Kwa hisani ya Gordon Kalulunga na Venance Matinya

TCRA WAENDELEA KUTOA ELIMU YA MABADILIKO YA KUTOKA KUTUMIA ANALOGI NA KUAHAMIA DIGITAL KWA WAKAZI WA MBEYA NA VITONGIJI VYAKE

Moja ya watumishi wa mamlaka ya mawasiliano nyanda za juu kusini Asajile akiwaelimisha wananchi wa eneo la kabwe kituo cha mabasi yaendayo maeneo mbali mbali ya jiji la Mbeya na wilayani umuhimu wa kutumia vifaa vya digital na kuachana na analogia

Wananchi wakiwa makini kusililiza mafunzo mafupi ya mabadiliko ya analogia na  kuingia digital


Hapa wananchi wakinyoosha vidole ili wajibu maswali yanayoulizwa na maafisa wa mamlaka ya mawasiliano kuwa tayari wameshaelea mabadiliko yanayokuja

Moja ya wananchi waliyojibu vizuri maswali eneo hilo akipokea zawadi ya simu  kwa ujumla zawadi mbali mbali zilitole eneo hilo